Elimu ya ujasiriamali kwa wanakikundi

Ujasiriamali ni nini? 

Neno Ujasiriamali linatokana na neno  Ujasiri + Mali = Ujasiriamali. 

Kama mjasiriamali ni vizuri sana kuwa na kumbukumbu za mapato na matumizi yetu ili kuepukana na matumizi yasiyo ya lazima au matumizi yasiyo na mpangilio. 

Taasisi ya Caring Hearts CAHE  wametoa Elimu ya Ujasiriamali kwa Kikundi Cha Faraja (FARAJA GROUP) ambacho kipo Mtaa wa Ngelewala Kata ya Mwangata Mkoani Iringa Kama utekelezaji wa Programu yake kutoa Elimu hiyo katika Vikundi vya kata zote za Manispaa ya Iringa. 

Elimu hiyoya Ujasiriamali  imetolewa na Ndugu  Jemida Kulanga ambapo amewasisitiza wanakikundi hao kuwa na nidhamu ya pesa kwani  kwa kufanya hivyo mitaji yetu itakuwa na uwezo wa kuleta faida. 

Endelea kutufuatilia kupitia Caring Hearts CAHE Ujasiriamali kwa Maendeleo ya Jamii zetu

Elimu ya Ujasilia mali kataka picha

Matukio katika picha