Caring Hearts (CAHE) organization participated in the Training on Advanced Fundraising Strategies, held from 2nd to 4th December 2025 at Kingsway Hotel, Morogoro Town. The training was organized by APN and brought together representatives from various organizations to enhance their fundraising knowledge and skills.
The organization was represented by Executive Director Mr. Oswald Abinery Kikoti and Fundraising Officer Mr. Hosian Patrick Kikoti. The training provided an excellent opportunity to strengthen participants’ understanding of advanced fundraising strategies, resource mobilization, and ensuring the sustainability of organizational programs. Caring Hearts (CAHE) organization values such capacity-building initiatives and is committed to applying the skills gained to improve its fundraising efforts and impact in the community.
Taasisi ya Caring Hearts (CAHE) ilishiriki katika Mafunzo ya Mikakati ya Juu ya Utafutaji wa Rasilimali, yaliyofanyika kuanzia tarehe 2 hadi 4 Desemba 2025 katika Hoteli ya Kingsway, Manispaa ya Morogoro. Mafunzo haya yaliandaliwa na APN na yalileta pamoja wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali ili kuimarisha ujuzi na maarifa yao katika utafutaji wa rasilimali.
Taasisi hiyo iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Taasisi Bw. Oswald Abinery Kikoti na Afisa Utafutaji wa Rasilimali Bw. Hosian Patrick Kikoti. Mafunzo haya yalitoa fursa muhimu ya kuongeza uelewa na ujuzi wa vitendo kuhusu mbinu za kisasa za utafutaji wa rasilimali, uhamasishaji wa fedha, na kuhakikisha uendelevu wa programu za taasisi. Taasisi ya Caring Hearts (CAHE) inaendelea kuthamini fursa kama hizi za kujengewa uwezo na itaweka katika vitendo maarifa yaliyopatikana ili kuimarisha juhudi zake za utafutaji wa rasilimali na mchango wake kwa jamii.




