Mkurugenzi wa Caring Hearts (CAHE) leo tarehe 08 Mei, 2023 amepata nafasi ya kutembelea Shirika la Namnyaki Maasai Girls and Women Organization (NAMGWO) kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika tasnia ya NGOs.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi wa CAHE Ndugu Oswald Abinery Kikoti, Mkurugenzi wa NAMGWO Mchungaji Paulo Ole Kurupashi pamoja na Katibu wa NAMGWO Ndugu Sekemi Ole Sandoni wameongea mambo mengi ikiwa ni pamoja na kushirikiana katika kuandaa Semina na kutoa elimu ya kukomesha Ukatili dhidi ya Wanawake, Vijana na Watoto Mkoani Iringa na Tanzania kwa Ujumla.
CAHE tunawashukuru sana NAMGWO kwa mapokezi mazuri.
“Tanzania Bila Ukatili Inawezekana”


 
  
  
  
  
 