Katika kuunga mkono Serikali na wadau wengine katika kampeni ya Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia, Taasisi ya Caring Hearts (CAHE) waliandaa semina kwa vijana kuhusu changamoto za sonona (Msongo wa Mawazo) ambayo ilifanyika katika Ukumbi wa Iringa Boma chini ya Mtaalamu wa Mambo ya Saikolojia Mchungaji Hasborn Myenda wa Iringa kwa ushirikiano na Mchungaji Tito Kilale.
Katika semina hiyo vijana walijengewa uwezo wa kutambua changamoto zinazotokana na msongo wa mawazo na jinsi msongo wa mawazo unavyoweza kusababisha matatizo mengi ya kimaisha ikiwemo ukatili wa kijinsia.
Vijana walifundishwa namna ya kutambua changamoto zinazowakabili mapema na jinsi ya kuzitafutia ufumbuzi kwa ajili ya ustawi wao.
Vijana walipokea kwa shukrani Mafunzo hayo kwani walipata uelewa wa kutosha kuhusu madhara ya msongo wa mawazo na jinsi ya kukabiliana nao ili kuondokana na ukatili wa kijinsia.
Tunatoa mwito na kuwakaribisha vijana wote wanaohitaji msaada wa kisaikolojia waweze kusaidiwa ili wasiingie kwenye changamoto zinazotokana na msongo wa mawazo.
Endelea kufuatilia tovuti yetu ya www.caringhearts.or.tz na katika Mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram.


 
  
  
 