Semina ya mahusiano yenye afya kwa vijana boma 29 okt 2022

Kutokuwepo kwa mahusiano yenye afya miongoni mwa vijana imekuwa ni changamoto inayoumiza hata kama inachukuliwa kama ni swala la kawaida tu. Kihalisia, vijana na hata watu wazima wanapenda mahusiano yenye afya kwa maana ya mahusiano mazuri kwa ujumla wake.

Aidha, mahusiano yasiyo na afya yamekuwa ni janga la kijamii miaka nenda rudi. Kwa sababu ya mahusiano yasiyo na afya jamii imeumia kwa kupoteza nguvu kazi pamoja na kutopata huduma stahiki kupitia wahanga wa mahusiano yasiyo na afya katika ngazi zote za watoa huduma serikalini, sekta binafsi pamoja na taasisi za dini.

Taasisi ya Caring Hearts (CAHE) – yaani Mioyo Inayojalia – imeanza kutoa semina mbalimbali zikiwemo zinazohusu uelewa wa kutosha kuhusu mahusiano miongoni mwa wanajamii ili kutatua changamoto zinazosababishwa na mahusiano yasiyo na afya.

Hivi karibuni Taasisi ya CAHE iliendesha semina kuhusu Mahusiano Yenye Afya kwa Vijana katika Ukumbi wa Makumbusho – Iringa Boma kwa lengo la kutoa Elimu ya Afya ya Mahusiano kwa Vijana.

Semina hiyo iliendeshwa na Mchungaji Tito Kilale bila kumumunya maneno huku akitoa mifano hai ya jinsi mahusiano yasiyo na afya yanavyoumiza si wahanga wa moja kwa moja tu, bali jinsi mahusiano yasiyo na afya yanavyochangia sana kudumaza ustawi na maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla wake.

Taasisi ya CAHE imeandaa mfululizo wa semina zinazohusu mahusiano yenye afya si kwa vijana tu, bali kwa watu wazima, waseja, wagane na wajane.

Ili kujua semina zinazotolewa na tarehe za kufanyika kwa semina hizo tafadhali tembelea tovuti ya Taasisi www.caringhearts.or.tz
au FaceBook: Caring Hearts – CAHE

Au wasiliana na Mkurugenzi Mtendaji wa CAHE kwa Simu Namba 0735 376 409

“Mahusiano Yenye Afya, Kwa Ustawi na Maendeleo yako”

Semina ya Mahusiano kataka picha